17 Julai 2014 - 20:53
 Lailatul-Qadr

lailatul qadri ni usiku wa pekee ambao ni kama zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake kwani kufanya ibada katika usiku huu ni sawa na kufanya ibada ya miezi elfu moja.


بِسْمِ اللهِ الرَّحْمنِ الرَّحِيم
إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ* وَمَا أَدْرَاكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ* لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ * تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍ *سَلَامٌ هِيَ حَتَّى مَطْلَعِ الْفَجْرِ

"Tumeiteremsha Qurani katika usiku huo wa Titulature-Qadr. Na nini kitakufahamisha wewe maana ya Laylatul-Qadr? Usiku wa laylatu! Qadr ni bora kuliko miezi elfu. Usiku huo huteremka Malaika na Jibrilu (A) pamoja na hukumu zote za mwaka mzima kwa idhini ya Mola wao. Amani (usiku) huo mpaka mapambazuko ya Alfajiri"

Usiku huo ni usiku ambao hubainishwa kila jambo la hekima. Mwenyezi Mungu anasema: "Kwa yakini tumeiteremsha (Quran) katika usiku uliobarikiwa; bila shaka sisi ni waonyao. Katika (usiku) huu hubainishwa kila jambo la hekima na maslaha" (44:3-4). Usiku huu ndio Mwenyezi Mungu huweka mambo ya viumbe wake mpaka mwaka mmoja. Kwa mfano, kila atakayezaliwa, atakaye kufa. atakaye tajirika, atakaye kuwa masikini, atakaye kuwa na cheo, atakaye dhalilika, atakaye shinda, atakaye shindwa, atakaye ongoka, atakaye kupotea, atakaye pona, atakaye kuwa mgonjwa, na mambo mengi kama hayo ambayo humsibu binadamu.
Amali nzuri usiku huo ni kusali, kutoa zaka, kutenda kila jambo zuri la khayri; kwani ukitenda usiku huu ni bora kuliko amali ya miezi elfu isiopo kati yao Laylatul-Qadr. Usiku huu huteremka Malaika pamoja na AR-RUUH ambaye ni Malaika alie adhimiwa kuliko Malaika wote, kwa amri ya Mwenyezi Mungu wanafika kwa Al-Imaam Al-Mahdi (A), na wanamwonesha kila alichokadiriwa yeye na watu wote na Mola, mwaka ujao mpaka Laylatul. Qadr ijayo.
Kama ilivyo katika hadithi ya Laylatul Qadr hii, juu ya utukufu wake, na jinsi inavyokuwa inayo manzila na cheo, lakini bado hatuijui, na maarifa ya kuwekwa hiyo siku, na siku gani kwa hakika hiyo haikubaynishwa. Lakini inatumainiwa kuwa ni moja katika usiku wa tarehe kumi na tisa (19), ishirini na moja (21), ishirini na tatu (23). ishirini na tano (25) na ishirini na saba (27); na labda zaidi inatumainiwa sana kuwa katika usiku wa tarene ishirini na moja na ishirini na tatu (21 na 23), Hadithi nyingi za Maimamu wetu (A.S.) zilizopokewa zinatilia nguvu sana kwamba Lay-latul-Qadr ni usiku mmoja katika usiku hizo mbili (21 au 23). Mara nyingi watu wamewaomba Al-Imaam (A) awaainishiye (dhihirishie) siku ipi katika hizo mbili? Imaam hakuainisha, na akajibu, "Itakudhuru nini ukifanya mambo mazuri (Ibada) usiku mbili hizi?".
Imepokewa kwa Imaam Al-Baaqir (A) kutokana kwa baba zake watukufu.(A.S.) kwamba wamesema hivi, "Mtume (S.A.W.) amekataza mtu kutojali usiku wa Ishirini na moja na Ishirini na tatu, na amekataza kulala mtu usiku hizo". Vile vile amesema (A) kwamba "Mtume (S.A.W.) alikuwa akikunja 'matandiko yake na akikaza kitambaa cha kiunoni (mshipi) katika siku kumi za mwisho wa mwezi wa Ramadhani (alikuwa akikesha kwa Ibada) na akiwafanya watu wake wa nyumbani wakeshe usiku wa Ishirini na tatu na akiwarushia maji usoni mwa wenye kulala. Na alikuwa Bibi Fatima (a.s) hamwachi mtu yoyote katika watu wake wa nyumbani kulala usiku huo, na akiwatibu kwa kula kidogo (akiwaeleza kama kula kidogo hupunguza usingizi; na ukila sana huleta usingizi mwingi), na akijiweka tayari kwa Ibada ya usiku tangu mchana.
Ala kulihali, usiku wa AI-Qdri haimfalii mtu kuupuuza kulala, bali akeshe kwa Ibada ya Mwenyezi Mungu kwa kusali, kutubia, kufanya dhikri (kutoa uradi) na kila amali za suna zilizowekwa na kupangwa kwa usiku huu. Usijidanganye nafsi yako kwa kusema nimechoka au ninaumwa kichwa na kuonesha uchovu. Kwa sababu haya yote hutokana na adui wetu mkubwa shetani, kukukosesha mafanikio na manufaa yote ya kheri za usika huu. Kama alivyosema Bibi Fatima (a.s), "Mwenye kunyimwa ni yule mwenye kujinyima kheri zote za usiku huu". Basi, ndugu zangu, msikose yote haya kwani hujui mwakani utakuwapo hai, upate kufidia uliyo yakosa !!
Maelezo na Utaratibu wa Amali za Laylatul Qadr
(1)Kuoga (Ghusl) usiku wa 19, 21 na 23. Ni bora uoge wakati linapozama jua, hata upate kusali sala ya magharibi na Isha kwa hiyo ghusli, lakini utawadhe pia.
(2)Ukeshe kucha usiku zote tatu za Laylatul-Qdri kuomba dua, kunyenyekea, kuomba kughufiriwa.
Imepokewa hadithi tukufu inayosema kwamba kila mwenye kukesha kucha Mwenyezi Mungu atamghufiria madhambi yake yote hata yakiwa kwa idadi ya nyota zote, au majabali, au kiasi cha maji ya bahari zote (utaghufiriwa dhambi zako binafsi na Mola, si za watu kama umemwibia mtu).
(3)Usali raka mbili katika usiku wa Laylatul-Qadr (19, 21, 23). Katika kila rakaa, baada ya Sura ya AL-
HAMDU, soma Sura (Qul-Huwal-Laah) mara saba na ukiisha maliza hiyo sala, hapo hapo soma mara sabini (70)
hivi; As-tagh-firul-Laa-ha wa Atuu-bu-Ilay-hi. Imepokewa hadithi tukufu inasema, 'Mwenye kuzisali hizi rakaa
mbili kama ilivyo elezwa. basi kabla ya kuondoka mahala pake Mwenyezi Mangu atamghufiria yeye na wazee wake.
(4)Usome usiku wa mwezi 19, 21 na 23 mara mia moja (100) . As-tagh-firul-laah rab-bee wa atubu-ilayh.
(5)Usiku wa 19 na 21.usome mara mia moja (100): Al laa-hum-mal-an, qata-lata, Ameeril-mu-mineen.
(6)Ufunue Qur’ani tukufu. uiweke wazi mbele mikononi mwako na usome dua hii: "Al-la-hum-ma in-nee as-alu-ka biki-taa-bikal, munzali wa maa fee-hi wa fee-his-mu-kal ak-baru wa as-maa-ukal hus-naa wa maa yukhaa fu wayur-jaa an taj-alanee min uta qaa-ika minan -naar". Baadaye uombe maombi yako yote.
(7)Tena uifunge Qur’ani na uiweke juu ya kichwa chako (Tahadhari isianguke) na useme maneno haya: "Al-laa-hum-ma, Bi-haqqi ha dhaal-qur’aan wa Bihaqi man ar sal-taho bih wa Bihaq qi kul-li mu-mi-nin ma-dah-tahu feeh wa Bi-haq-qika, alay-him, falaa ahada a’ rafu Bi-haq-qika minka". Tena sema mara kumi hivi: Bika yaa Allaahu; mara kumi, Bi-Muhammadin (S.A.W.); mara kumi, Bi-Aliy-yin (a.s); mara kumi, Bi-Faa-timata (a.s); mara kumi, Bil-Hasani (a.s); mara kumi, Bil-Husaini (a.s); mara kumi, Bi-Aliy-yibnil-Husain (a.s); mara kumi, Bi-Muhammadi bin-Aliy-yln (a.s); mara kumi, Bi-Jafa-ribni-Muhammadin (a.s); mara kumi, Bi-Muusabni-Jafarin (a.s); mara kumi Bi-AIiy-yibni Muusa (a.s); mara kumi, Bi-Muhammadi-bni-AIiy-yin (a.s); mara kumi, Bi-Aliy-yibni-Muhammadin (a.s); mara kumi Bil-Hasanibnl-Aliy-yin (a.s) Hapo inuka katika hali ya kusimama mkono mmoja umeikamata Qurani ilioko juu ya kichwa, basi sema mara kumi Bl-Huj-ja (a.s); tena taja moyoni haja zako zote na utake kwa Mwenyezi Mungu baraka ya usiku huu wa Lay-latu Qadri.
(8)Kumzuru Imaam Husain (A) katika usiku wa Lay. Latul-Qadri. Imepokewa hadithi tukufu inayosema kwamba, "Huita muitaji (Malaika) kutoka mbingu ya saba kwenye. Arshi hivi, 'Bila shaka Mwenyezi Mungu amemghufiria mwenye kuhudhuria (kuizuru) kaburi tukufu la Imaam Husain (a.s)". Basi zipo Ziyara mahsusi nyingi katika vitabu vya Ziyara, na ukisoma Ziyara mashuhuri kwa jina la Ziyaaratul Waaritha itatosha. Ziyara hii inaanzia kwa maneno haya: "As-salaamu alay-ka, yaa waa-ritha Aa-dama saf’wa-til-Iaah"[7]
(9) Usali rakaa mia (100) katika kila usiku wa 19, 21 na 23. Kusali huko kuna thawabu mno, na bora kusali hivi. Katika kila rakaa, baada ya sura ya "AL-HAMDU", soma sura ya -QUL-HUWAL-LAAHU mara kumi. Vile vile unaweza kusali raka mia hizo kwa (kukidhi) kulipa sala zako za fardhi uloziwacha kusali kwa udhuru fulani fulani muda wa mwaka; kwa mfano ikiwa unadaiwa sala ya siku sita itakuwa rakaa mia moja na mbili (102) Kuanzia sala ya adhuhuri ya siku ya kwanza mpaka asubuhi ya siku ya saba.
HADHARI Sala ya sunna yeyote haijuzu kusali kwa mafungu zaidi ya rakaa mbili, utazisali kama sala za asubuhi; vile vile huwezi kusali kwa Jamaa kabisa, isipokuwa sala za Idi na Salatu-Istisqaa" (Sala ya kuombea mvua tu).
(10) Usome usiku wa mwezi ishirini na tatu (23) Sura za Qurani zijazo: AL-ANKA-BUUT. (J.20: S.29), Ar-Ruum (J.25: .30), na AD-DU-KHAAN (J25:S.44). Katika hadithi tukufu amesema Imaam As-Sadiq (A): "Ninaapa, mwenye kuzisoma zile sura mbili (za mwanzo) usiku huu, ni mtu wa Peponi"
AMALI ZA KUMl YA MWISHO WA MWEZI
(l)Kuanzia usiku wa kumi la tatu mpaka mwisho wa mwezi mtukufu (usiku wa 21 mpaka mwisho) soma dua hii kila usiku. "A'udhu bi-jalali waj-hikal-Kareem, an yan-qadhi-ya an-nee shahru Ramadhan au yatlual-Fajru min lay-latee ha-dhi-hee walaka qi-balee dhan-bun au fabi-atun tuadh-dhi-buni alayh".
(2) Imaam Zaynul-Abedeen (A), "Imaam wa nne, alikuwa akisoma dua hii usiku wa ishirini na saba (27) kila mara, nayo ni hii: al-laa-hum-mar-zuq-nee at tajaa-fiya an daa-ril-ghu-ruur wal-inaa-bata Ilaa daa-ril-khu-luud wal is-tia-dada lil-mawti qabla hu-luu-lil-fawt.
(Ewe Mola wangu nipe uwezo wa kujitenga na mambo usiyoyapenda yenye kunidanganya humu (duniayani) na nifanye mambo mema ya kuniokoa huko akhera na adhabu yako, na nijiweke tayari kwa kufa kabla haikunijia mauti, (maana yake nifanye amali njema hata ikinijia mauti nisiwe na wasiwasi ya kukosa kutubia).
Usiache kuoga "GHUSL" usiku huu, na kukesha pia kwa Ibada, kama unaweza.
(3) Usome Dua ya Al-Widaa (ya kuuaga mwezi mtukufu wa Ramadhani) katika usiku wa mwisho, kama ilivyopokewa katika hadithi ya Al-Imaam Jaafar bin Muhammad As-Sadiq (a.s) Imaam wa sita; nayo ni hii: Al-laa-ham-ma laa tajal-hu aa-kbiral-ahdi min siyaa-mee li-shah-ri Ramadhan wa audhu bika an-yat-lua fajru haa dhi-hi?-lay-lati il-laa wa qad ghafarta-lee. Basi Mwenyezi Mungu atakughufiria kabla ya asubuhi na atakujalia na kuruzuku utubiye madhambi yako.
Haya yote ni badhi ya dua na sala zilizopokelewa katika hadithi tukufu, na mwenye kutaka zaidi atapata katika vitabu vya Dua na Ziyara kama Mafaateehul-Jinaan na zinginezo.